
Israel imesema wanajeshi wake, wametekeleza mashambulizi ya angaa Kusini mwa Lebanon, baada ya wapiganaji wa Hezbollah kuwashambulia kwa makombora.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, amesema, aliliagiza jeshi kuwashambulia wapiganaji wa Hezbollah na kuharibu ngome zao, Kusini mwa Lebanon.
Jeshi la Israeli, linasema limefanikiwa kuzuia makombora matatu yaliyorushwa kulenga mji wa Metula siku ya Jumamosi asubuhi, lakini hakuna aliyejeruhiwa.
Hii ni mara ya kwanza kwa mashambulio kati ya Israeli na Lebanon, tangu kupatikana kwa mkataba wa usitishwaji vita mwezi Novemba mwaka uliopita.
Hat hivyo, kundi la Hezbollah, limekanusha madai ya Israeli, na kusema ni mbinu ya jeshi la Israeli kutafuta mbinu za kuendelea kuwashambulia.