Jeshi la Israel limetangaza kuwa naibu kamanda wa kikosi na mwanajeshi mmoja wameuawa na wengine 3 kujeruhiwa vibaya katika mapigano kusini mwa Lebanon na kufanya idadi ya wanajeshi za Israel waliouawa jana Jumanne kuwa 3 na wengine 20 kujeruhiwa katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
Ni baada ya vyombo vya habari vya Israel kufichua kuwa naibu Kamanda wa Battalion 9308, Meja Aviram Harib (umri wa miaka 42), ameuawa katika vita kusini mwa Lebanon.
Awali vyombo vya habari vya Isarel vilikuwa vimetangaza kuwa wanajeshi wengine wawili wa utawala huo wameangamizwa huko Gaza. Vilevile wanajeshi wengine 20 wa utawala huo walijeruhiwa jana katika vita na wanamapambano wa Lebanon na Gaza.
Siku tatu zilizopita jeshi la Israel lilikiri kuwa, Kamanda wa Kikosi cha 401 cha jeshi la utawala huo ameuawa na wanamuqawama wa Palestina kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, jeshi la Israel limethibitisha.

Kwa mujibu wa jeshi la Israel, Ehsan Daqsa aliuawa baada ya kifaru chake kupigwa na mabomu katika mji wa Jabalia katika Ukanda wa Gaza Jumapili iliyopita.
Ripoti zinasema kuwa, wanajeshi kadhaa wa Kizayuni waliangamizwa katika operesheni hiyo.