Kufichuliwa kwa faili la sauti ya rais wa Chuo Kikuu cha Michigan kunaonesha kuanzishwa sera za kibaguzi dhidi ya wanafunzi wa Kiislamu na Waarabu katika jamii za Magharibi.
Mnamo Oktoba 7 mwaka huu, muungano wa mashirika yanayounga mkono Palestina katika Chuo Kikuu cha Michigan, unachojulikana kama Muungano wa Tahrir, (Muungano wa Ukombozi) ulifichua faili la sauti iliyorekodiwa iliyohusishwa na Santa Ono, rais wa chuo hicho kikuu, kwenye mitandao ya kijamii.
Katika faili hiyo, inasikikka sauti ya mwanamume mmoja akizungumzia shinikizo kutoka kwa “makundi yenye nguvu” na vitisho vya kukatwa ufadhili wa shirikisho iwapo chuo hicho kikuu hakitazingatia suala eti la kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi.
Muungano wa Tahrir haukutoa maelezo kuhusu jinsi ulivyopata faili hilo au wakati na mahali pa kutayarishwa kwake.
Kwa mujibu wa Ahmad Ibsais, mwandishi wa uchambuzi huu, tatizo kubwa ni kwamba chuo kikuu hakina wajibu wa kulinda usalama na kuwahami wanafunzi wa Kiislamu na Kiarabu.

Ripoti hiyo inasema, baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Michigan kuanza maandamano na kuwatetea watu wa Gaza dhidi ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel, kwenye kampasi ya chuo hicho, vitendo vya kibaguzi vya chuo kikuu vilionyesha sura yake mbaya zaidi. Inasema, mara nyingi polisi wa chuo kikuu waliingilia kati kutawanya maandamano ya amani na migomo ya wanafunzi Waislamu, na wanafunzi walipigwa na kukamatwa na kunyunyiziwa pilipili, na kwamba hijabu za wanafunzi wa kike pia zilikuwa shabaha ya mashambulizi hayo.
Hali hii haihusu Chuo Kikuu cha Michigan pekee. Katika kipindi cha miezi sita pekee, zaidi ya watu 3,000 wamekamatwa kwa kuunga mkono Palestina kwenye vyuo vikuu kote nchini Marekani. Vyuo vikuu vya Marekani ambavyo wakati mmoja vilikuwa watetezi wa uhuru wa kujieleza, sasa vimekuwa mazingira ya chuki dhidi ya wanafunzi wa Kiislamu na Waarabu na washirika wao.