Wanafunzi: Marufuku ya Hijabu Ufaransa ni ‘Ubaguzi wa Rangi na Chuki Dhidi ya Uislamu’

Chama cha Wanafunzi Waislamu wa Ufaransa (EMF) kimelaani vikali pendekezo la sheria inayopiga marufuku uvaaji wa Hijabu katika mashindano ya michezo, likiitaja kuwa “ya kibaguzi, ya chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) na ya ubaguzi wa kijinsia.”