
Hapo awali waliondoka mwezi Juni mwaka jana kwa misheni ya siku nane, Butch Wilmore na Suni Williams waliona muda wao wa kukaa ukiongezwa baada ya kugunduliwa kwa hitilafu kwenye chombo kilichowapeleka kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS). Wamerejea nchi kavu Jumanne, Machi 18, baada ya kutua salama kwenye ufuo wa Florida ndani ya chombo cha anga za juu cha Crew Dragon kutoka kwa kampuni ya SpaceX ya Elon Musk.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Baada ya zaidi ya miezi tisa kukwama kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS), wanaanga wawili wa Kimarekania wamerejea Duniani Jumanne, Machi 18, mwisho wa sakata ya anga na kisiasa iliyouteka ulimwengu. Baada ya safari ya saa 17, chombo cha anga za juu cha SpaceX kinachomilikiwa na Elon Musk kimetua kwa upole kwenye pwani ya Florida, kikipunguzwa kasi na parachuti nne zenye nguvu.
Suni Williams wa Marekani na mshirika wake Butch Wilmore waliandamana katika safari yao ya kurejea na mwanaanga mwingine wa Marekani, Nick Hague, pamoja na mwanaanga wa Urusi, Aleksandr Gorbunov. Wote wanne wamelakiwa na kundi la pomboo lililozunguka chombo hicho kilichokuwa kikielea. “Ni tukio la ajabu!” ” ameshangaa Nick Hague, ambaye alikuwa akiongoza chombo hiki, akielezea “tabasamu kubwa” za wenzake.
Kisha chombo cha Crew Dragon kilitolewa majini na abiria wake wametolewa kwa uangalifu na kuwekwa kwenye machela. Baada ya uchunguzi wa awali wa kimatibabu, walipaswa kusafirishwa jioni hadi Houston, Texas, ambako wataunganishwa na familia zao na kisha kufuatilia programu ya ukarabati wa nguvu ya uvutano ya Dunia.
Kushindwa
Butch Wilmore na Suni Williams, ambao walianza safari yao mnamo mwezi Juni mwaka jana kwa safari ya siku nane, waliona kukaa kwao angani kukiendelea baada ya kugunduliwa kwa hitilafu kwenye chombo cha anga za juu cha Boeing Starliner kilichowabeba. Matatizo haya ya kiufundi yalisababisha NASA kuamua, wakati wa kiangazi, kurudisha chombo hicho bila kitu na kukabidhi urejeo wao kwa kampuni ya Elon Musk ya SpaceX, chombo kilichotengenezwa na Boeing.
Safari yao imewafanya wasikilizwe na umma, lakini hivi majuzi, pia imevutia umakini wa kisiasa, huku Rais wa Marekani, Donald Trump akimshutumu mtangulizi wake Joe Biden kwa “kuwatelekeza” watu hao wawili wasio na bahati kwa makusudi na kuahidi “kuwaokoa”. “Ahadi imetekelezwa,” Ikulu ya White House imejigamba siku ya Jumanne kwenye mtandao wa X, ikisifu jukumu lililofanywa na Elon Musk.
Mjasiriamali huyo tajiri ambaye amekuwa mshirika wa karibu wa Donald Trump, hivi majuzi alidai kwamba angeweza kuwarudisha wanaanga hao wawili muda mrefu uliopita, bila kutaja jinsi gani. Matamshi haya yalizua mtafaruku katika jumuiya ya anga, kwa sababu mpango uliowaruhusu kurudi ulikuwa umeanzishwa vyema kabla ya mrejesho ya Republican kuchukuwa mamlaka ya uongozi wa nchi.