Wamisri wakusanyika mbele ya Kivuko cha Rafah, wakipinga kuhamishwa Wapalestina wa Gaza

Raia wa Misri walikusanyika jana Ijumaa mbele ya kivuko cha mpakani cha Rafah na Ukanda wa Gaza wakipinga pendekezo la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kuwafukuza Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza na kuwapeleka nje ya nchi yao.