
Huko Mashariki mwa DRC, naibu waziri mkuu anayehusika na masuala ya ulinzi, amefanya ziara mjini Uvira katika jimbo la Kivu kusini ili kujionea hali ya mambo baada ya M23 kuteka mji wa Bukavu na baadhi ya vijiji vya jimbo hilo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Akisindikizwa na mratibu wa kitaifa wa hifadhi ya ulinzi wakitaifa luteni Jenerali Padiri Bulenda David, naibu waziri mkuu akiwa pia waziri wa ulinzi Guy Kabombo Mwadiamvita amesema amefika kuwatia moyo watu wake kwenye mapambano akiwahimiza pia kuwa hodari katika ulinzi wa ardhi ya Kongo.
“Nimefika hapa kwa niaba ya Rais Felix Tshisekedi Tshilombo. Amenituma niwaambiye kwamba tuko pamoja. Nafika kujionea hali yenu na baadae nitampa ripoti.” alisema Guy Kabombo Mwadiamvita
Naibu waziri mkuu huyo pia amekutana watu mbalimbali wakiwemo makamanda wa jeshi la FARDC, wapiganaji Wazalendo, na viongozi wa tabaka mbalimbali za kisiasa, na baadae kumteua kamanda mpya wa jeshi la FARDC jenerali Dunia Rashidi.
Uvira ni mji wa pili wa jimbo la Kivu kusini ambapo kwa sasa unahifadhi kwa muda taasisi za serikali ya jimbo la Kivu kusini wakati huu ambapo mji wa Bukavu unadhibitiwa na M23.
Wakazi wa Uvira wanamtazamo gani kuhusu juhudi za kutafuta amani mashariki mwa DRC ? Baadhi wanaeleza:
“Kwanza tunashukuru ujio wake hapa. Tunamwomba kwamba vyote ambavyo havijakuwa sahihi kati ya Wazalendo na FARDC vikamilishe … Tunataka waungane ili wasonge mbele wateke tena Kamanyola na mji wa Bukavu … Kwa siku za usoni wakimbize adui na nihapo raia watafanya kazi kwa amani”
Wakazi wengine wanatarajia matokeo chanya kutokana na mazungumzo yanayopangwa kati ya serikali ya Kongo na M23 Jumatano ijayo huko Doha Nchini Qatar, kwa ajili ya kurejesha amani mashariki mwa DRC.