
Mtazamo wa mzigo mkubwa wa madeni unaozikumba nchi maskini unahitaji kurekebishwa haraka ili kuepusha mizozo mingi, viongozi wa Afrika walmesema siku ya Alhamisi wakati wakizindua mpango unaolenga kupunguza matatizo yao ya mikopo.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Rasimu hiyo ambayo ilitiwa saini kando ya mkutano wa mawaziri wa fedha wa G20 mjini Cape Town, inatoa wito wa kufanyiwa marekebisho mfumo wa kimataifa wa utoaji mikopo ili kufungua unafuu wa madeni na masharti mazuri ya kukopa kwa nchi za Afrika. Unaojulikana kama Mpango wa Kulipa Madeni ya Viongozi wa Afrika (ALDRI), utaongozwa na timu ya watu saba, wakiwemo marais watano wa zamani, makamu wa rais na waziri mkuu.
“Zaidi ya nusu ya wakazi wa Afŕika wanaishi katika nchi zinazotumia zaidi malipo ya riba kuliko elimu, afya au tabianchi,” amebainisha ŕais wa zamani wa Mauŕitius, Ameenah Gurib-Fakim. “Nchi nyingi za Afrika zitahitaji msamaha mkubwa wa madeni ili kufungua ufadhili unaohitajika kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa 2030 kwa malengo ya Mkataba wa Paris,” ameongeza. Afrika Kusini, ambayo inashikilia urais wa zamu wa G20 mwaka huu, inataka kusaidia nchi zinazoendelea kiuchumi kufikia ulipaji wa madeni yao.
Hii ni mara ya kwanza kwamkutano wa G20 kufanyika barani Afrika, lakini mijadala imetawaliwa na mmomonyoko wa siasa za pande nyingi na kutokuwepo kwa maafisa wakuu wa Marekani. Ofisi ya rais inatoa “fursa ya kipekee ya kuongoza malipo ya msamaha wa madeni,” amesema makamu wa rais wa zamani wa Nigeria, Yemi Osinbajo. Kulingana na ALDR, nchi za kipato cha chini na kati zimetumia kiasi kikubwa cha dola trilioni 1.4 kulipia deni lao, ikijumuisha malipo ya riba ya dola bilioni 406.
Kupanda kwa gharama za deni kunakula fedha ambazo zingeweza kutumika kupambana vyema na umaskini, kushughulikia majanga ya hali ya hewa na changamoto nyinginezo, wakuu wa nchi na serikali wamesema. Kulingana na IMF, wastani wa uwiano wa madeni wa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara ulikuwa umefikia rekodi ya juu ya karibu 60% ya pato la taifa kufikia mwisho wa mwaka 2022. Mwaka jana, Zambia ilitia saini mkataba wa madeni na wakopeshaji wake wa kigeni, ambao ulisaidia kupunguza mzigo wa kifedha kwa taifa la kwanza la Afrika kushindwa kulipa baada ya mlipuko wa UVIKO.