Wakuu wa nchi za SADC wanakutana kwa njia mtandao kujadili hali ya DRC

Viongozi kutoka nchi wanachama za SADC wanakutana kwa njia mtandao kujadili mzozo wa mashariki ya DRC ambapo pia wanafanyia tathmini ya ujumbe wa kijeshi ambapo baadhi ya wanajeshi waliuawa na waasi mwaka uliopita.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu ndio wa hivi punde kufanyiwa na wakuu wa nchi za (SADC) kuhusu mzozo wa DRC umekuja siku moja kupita baada ya nchi ya Angola kutangaza kwamba mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Kinshasa na waasi wa M23 yataanza wiki ijayo.

Waasi wa M23 wameripotiwa kuendelea kuteka baadhi ya maeneo yenye utrajiri wa madini mashariki ya DRC kuanzia mwezi Januari mwaka huu ambapo pia wameingia katika Miji ya Goma na Bukavu.

Viongozi hao wanajadili kuhusu hali ya kibinadamu mashariki ya DRC pamoja na kuangazia upya majukumu ya wanajeshi wa SADC nchini humo (SAMIDRC), kulingana na katibu Mkuu mtendaji wa SADC Elias Magoso.

Wanajeshi 14 wa Afrika Kusini wameuawa katika mapigano mashariki ya DRC tangu mwezi Januari mwaka huu. Wengi wanajeshi hao walikuwa sehemu ya ujumbe wa SAMIDRC lakini wawili kati yao walikuwa wametumwa katika kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Maofisa wengine watatu wa jeshi la Malawi waliokuwa sehemu ya ujumbe wa SADC pia waliuawa mashariki ya DRC.

Ujumbe wa SADC ulitumwa mashairiki ya DRC mwezi Desemba mwaka wa 2023 kujaribu kuisaidia serikali ya DRC, mwanachama wa SADC kurejesha amani na usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *