Wakuu wa EAC na SADC waongeza kasi ya kujaribu kusuluhisha mzozo wa DRC

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na ile ya SADC, wameongeza kasi ya kujaribu kusuluhisha mzozo wa mashariki mwa nchi ya DRC, ambapo wametangaza kuongeza timu ya wapatanishi kufuatia kikao chao cha Jumatatu ya wiki hii.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katika kikao chao, mbali na wapatanishi wa awali, rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, waliwaongeza viongozi wengine katika timu ya upatanishi akiwemo rais wa zamani wa Afrika Kusini, Kgalema Motlante, rais wa zamani wa jamuhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba Panza.

Amejumuishwa pia rais wa zamani wa Ethiopia, Sahle Work Zewde anayechukua nafasi ya waziri mkuu wa zamani, Hailemarim Desalegn.

William Ruto ni rais wa Kenya na mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Hali mashariki ya DRC haibadiliki, inaendelea kuwa mbaya na inaleta hofu sio tu kwetu lakini katika ukanda wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC kwa sababu mzozo huu unaweza kusambaa kwenye nchi nyengine.’’ Alisema Rais Ruto.

Wanajeshi wa DRC wamekuwa wakipambana na waasi wa M23 walioripotiwa kuingia katika Miji ya Goma na Bukavu.
Wanajeshi wa DRC wamekuwa wakipambana na waasi wa M23 walioripotiwa kuingia katika Miji ya Goma na Bukavu. © Janvier Barhahiga / AP

Wachambuzi wa siasa za ukanda wanamtazamo gani kuhusu hatua hii? Mali Ali amezungymza nasi akiwa Ufaransa.

“Kuwepo kwa wapatanishi ni kitu kimoja pia lakini pia kufahamika kiini au mzizi wa mzozo wenyewe pia ni kitu kikubwa.’’ Alisema Mali Ali.

Tangu waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda kuchukua miji muhimu mashariki mwa Congo, jumuiya hizi mbili zimekuwa zikijaribu kuzipatanisha pande hizo bila mafanikio.

Haya yanajiri siku chache kupita tangu Angola iliyokuwa mpatanishi wa mzozo wa mashariki mwa Congo itangaze kujiondoa, huku pia juma lililopita rais Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame alikutana Qatar na kukubaliana kudhughulikia mzozo unaoendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *