
Msemaji wa mamlaka ya jiji la Berlin amesema wahusika tayari wamewasilisha maombi ya kuomba hifadhi ambayo yanachunguzwa kwa mujibu wa sheria.
Jumatatu, Mahakama ya Berlin ilitoa uamuzi wa dharura kwamba kuwarudisha wakimbizi hao watatu kutoka Somalia ilikuwa ni hatua isiyo halali.
Mahakama ilisema bila ufafanuzi kuhusu ni nchi gani ya Umoja wa Ulaya inayowajibika kushughulikia maombi yao ya hifadhi, watu hao hawapaswi kukataliwa kuingia nchini na kurudishwa walikotoka.
Awali, wakimbizi hao watatu, waliokuwa wamekimbia kutoka nchini mwao Somalia na kufika Ujerumani, walirudishwa Poland.