Wakimbizi wa Palestina waendelea kutumia eneo la Netzarim baada ya Israel kuondoka kikamilifu

Vyombo mbalimbali vya habari vimetangaza kuwa, baada ya wanajeshi wa Israel kutoka kwenye eneo la Netzarim huko Ghaza kama yalivyosema makubaliano ya kusimamisha vita, hivi sasa wakimbizi wa Palestina wanaendelea kuvuka eneo hilo na kurejea kwenye maeneo yao.