Wakimbizi wa mapigano ya Goma wanahitaji msaada wa dharura ,yasema MSF

Shirika la kimataifa la madaktari wasio na mipaka, MSF waathiriwa wa mzozo wa M23 na vikosi vya Congo,wameanza kuondoka kambini kurudi nyumbani ila hali ya kibinadaam wanayokutana nayo inaogofya

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Shirika la kimataifa la madaktari wasio na mipaka,MSF limetoa wito kwa mashirika ya kimsaada ,kuboresha hali ya  msaada wa kibinadaam kwa maelfu ya wakimbizi  waliokuwa wamekimbia mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,ambao wameanza kurejea nyumbani kwa uwingi.

MSF inasema watu hao wanaorejea wanakumbwa na hali ya wasi wasi , hali ngumu ya kimaisha ,wengi wakiwa hawana chakula  na kukosa huduma za afya.

Hatari inayohusishwa na ukosefu wa chakula ni kubwa.isitoshe,kuna hatari ya majanga ambayo yamekuwa Goma,kuna haja ya kuimarisha msaada wa kibinadaam na kusikitisha ,kuna mashirika machache ya kimsaada ambayo yanafanya kazi kwa sasa eneo hili,” alisema Anthony Kergosien,mkuu wa huduma za MSF za muda eneo la Goma.

MSF imesema imebidi kubadili mbinu ya kutoa msaada haswa za afya ambazo zinahitajika kwa dharura kwa sasa.

Soma piaDRC: Dolla Bilioni 2.54 zinahitajika kwa ajili ya misaada ya kibinadamu

Kando na kutoa dawa ,vifaa vya kimsingi  na kuwatuma wahudumu wa afya kwenye vituo kadhaa eneo la Nyiragongo na Masisi ,MSF pia imeweka vituo vya afya ya kuhamishwa katika maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi.

“ Kila mahali ,tumekuta hali inayofanana,vituo vya afya ambavyo tayari havikuwa vinatumika ipasavyo kabla mzozo huu ,vilihamwa,kuharibiwa au kuporwa.Na ni vituo ambavyo vinatarajiwa kutumika sasa ,kuna hatari ya magonjwa  ya Kipindu Pindu,MPOX na Surua ambayo tayari yalikuwa yameripotiwa,” alisema Anthony.

Katika mji Sake ,MSF ambao ni njia inayowaunganisha  watu wanaoenda Masisi ,Kitchanga na Kivu Kusini imebidi kujenga kituo cha kuwatibu wagonjwa wa Kipindu Pindu ambao wameongezeka.

 “Imebidi kufanya marekebisho kwenye kituo cha afya ambacho kilikuwa kimeharibiwa wakati wa mapigano.Tumejenga pia kituo cha kutibu Kipindu Pindu,ambacho kinatumika kuwatibu wagonjwa wasiopungua 20 kila siku.Isitoshe kuna wagonjwa 200 wengine wanaonekana kila siku ,wakiwa na matatizo ya kupumua ya kuharisha ,wale wa MPOX na waathiriwa wa dhulma za kingono,” alielezea Anthony.

Maelfu ya raia wa DRC wamepoteza makazi yao kutokana na mashambulio ya waasi.
Maelfu ya raia wa DRC wamepoteza makazi yao kutokana na mashambulio ya waasi. © JOSPIN MWISHA / AFP

Kando na huduma za afya ,wenyeji pia wanahitaji msaada wa kifedha,wakimbizi hao wanaorejea  hawana pesa ,hawawezi kufanya shughuli za kilimo au vifaa.

“Nilikuwa katika eneo la  Kabati  kwa wiki moja sasa. Kuna Amani ila njaa ni hatari hapa, tunahitaji dawa,wengi wetu tunaumwa,kuna watoto wengi wanaoendesha,” alisema mmoja wa wakimbizi kwa jina  Bigirimana, ambaye amekuwa katika kambi ya Bulengo kwa miaka miwili.

Kabla mapigano ya Januari ,Goma ilikuwa ni makao ya watu milioni mbili na tayari ilikuwa na wakimbizi 650,000 ambao ni waathiriwa wa machafuko ya kila mara ya waasi ,makundi yenye silaha na vikosi vya serikali.