Wakati wa uwasilishaji wa Bajeti Kuu ya Serikali katika Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema uchumi wa Zanzibar unakadiriwa kukua kwa wastani wa asilimia 7.3 mwaka 2025, ukilinganishwa na asilimia 7.1 mwaka 2024.
Miongoni mwa viashiria vya ukuaji huo ni ongezeko la watalii kwa asilimia 12.6 kutoka 736,755 mwaka 2024 hadi 829,929 mwaka 2025. Ukuaji huu unatarajiwa kuchochewa na usimamizi madhubuti wa sera za kifedha pamoja na kuimarika kwa upatikanaji wa nishati ya mafuta na gesi, hatua inayolenga kupunguza gharama za nishati hizo kwa wananchi.