Wakati taifa na wakazi wa Kanda ya Ziwa wakisubiri kwa hamu uzinduzi wa Daraja la JPM lililojengwa juu ya ziwa Victoria kati ya Busisi wilayani Sengerema na Kigongo wilayani Misungwi, wafanyabiashara wa maeneo hayo wameeleza wasiwasi wao mkubwa kuhusu shughuli zao kwenye eneo hilo.
Wanadai kuwa kuondolewa kwa vivuko na kupungua kwa usafiri wa magari yanayosimama kwenye maeneo hayo kumeathiri biashara zao kwa kiasi kikubwa na kusababisha kuporomoka kiuchumi.
Hata hivyo wakazi hao wa Mkoa wa Mwanza wamesifu juhudi za Serikali huku wakimuomba Rais na mamlaka husika kujenga vituo vya mabasi na masoko ili kuvutia watu wengi na hivyo kuendeleza shughuli za kibiashara katika maeneo hayo.
#azamnewsupdates
✍Innocent Aloyce
Mhariri| @official_jennifersumi