Wajumbe wa Urusi watua Istanbul kwa mazungumzo na Ukraine (vyombo vya habari vya serikali)

Ujumbe wa Urusi umewasili Istanbul kwa mazungumzo na Ukraine, shirika la habari la serikali ya Urusi Ria Novosti limeripoti. “Wajumbe wa Urusi wametua” huko Istanbul, chanzo cha habari kilichonukuliwa na shirika hili kimesema, kulingana na shirika la habari la AFP.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine anatazamiwa kukutana na kiongozi wa Uturuki Erdogan mjini Ankara kujadili mazungumzo na Urusi, afisa wa Ukraine ameliambia shirika la habari la AFP. Wataamua kwa pamoja juu ya “hatua zinazofuata” zitakazochukuliwa ili kupunguza mzozo nchini Ukraine.

Ni juu ya Urusi kuchukua hatua zinazofuata na Ukraine, anasema Mark Rutte

Ni juu ya Urusi kuchukua “hatua zinazofuata” katika mazungumzo na Ukraine, Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte amesema siku ya Alhamisi.

“Ni jambo liko wazi, ni Urusi kuchukuwa uamuzi,” amesema alipowasili Antalya, Uturuki, kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa NATO.

Ni yapi madai ya Kyiv na Moscow?

Tangu mwanzo wa uvamizi, Vladimir Putin amedumisha matakwa ya hali ya juu. Anasisitiza kwamba mchakato wa suluhu lazima ushughulikie “sababu kuu” za mzozo, kwanza kabisa nia ya Ukraine ya kujiunga na NATO, na pia anadai kuunganishwa kwa mikoa minne ya kusini na mashariki mwa Ukraine ambayo ambayo Urusi inadhibiti kwa sehemu (Donetsk, Lugansk, Kherson, Zaporizhzhia) na peninsula ya Crimea, mnamo mwaka 2014.

Ukraine inaendelea kudai kuondolewa kabisa kwa wanajeshi wote wa Urusi kutoka katika eneo lake. Na Volodymyr Zelensky anasisitiza wazi kwamba kyiv haitatoa Crimea, kwa sababu Katiba ya Ukraine inasema kuwa ni sehemu ya eneo lake. Kwa upana zaidi, Volodymyr Zelensky anatoa wito kwa washirika wake kutoa “dhamana ya usalama” kwa Ukraine ili kuzuia Urusi kuivamia tena baada ya makubaliano ya amani kufikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *