
Maafisa wa Marekai na Ukraine, wamekutana na kufanya mazungumzo kwa kifupi mapema leo nchini Saudi Arabia, siku moja baada ya mazungumzo mengine kama hayo na Urusi kumalizika bila mwafaka kuhusu mkataba wa usitishwaji vita.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Ripoti za ndani zinasema, hakuna makubaliano yaliyopatikana, katika hatua hii ya mazungumzo, huku Urusi ikiitaka Marekani ambaye ni msuluhishi, kuishinikiza Ukraine, kukubali mkataba mpya kuhusu matumizi ya Bahari nyeusi, ili kuinufaisha Moscow kuendelea kusafirisha bidhaa zake.
Hata hivyo, baada ya mazungumzo kati ya maafisa wa Marekani na Ukraine, ripoti kutoka Kiev kuwa kilichokubaliwa kati ya pande hizo mbili, kitaelezwa baadaye.
Ukraine imeendelea kuishtumu Urusi kwa kutatiza jitihada za kusitisha vita, na kuendelea kushambulia miundo mbinu yake ya nishati, licha ya kukubali kuachana na mashambulio hayo baada ya mazungumzo ya simu kati ya rais Donald Trump na Vladimir Putin.
Rais Trump, ameenndelea kushinikiza mkataba wa kusitisha vita nchini Ukraine kwa siku 30, na hatimaye, kumalizika kwa uvamizi wa urusi katika nchi hiyo jirani, ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka mitatu sasa.
Mazugumzo haya yanalenga kupata mwafaka wa usitishwaji vita, pendekezo ambalo Ukraine imekubali, lakini Urusi, haijaafiki.