
Dar es Salaam. Wanawake wanaofanya ujasiriamali na biashara wametakiwa kijitathimini kuhusu changamoto walizonazo katika ufanyaji biashara bila ya kujionea aibu.
Hayo yamesema na mwezeshaji Asha Sinare, wakati akitoa mada katika mkutano wa kuwajenga uwezo wanawake wajasiriamali uliandaliwa na Mtandao wa Jinsia (TGNP) kwa kushirikiana na benki ya Stanbic.
Asha ambaye mtaalamu wa rasilimali watu, amesema katika biashara kuna mambo mengi ikiwemo suala la kutojali muda , kuahidi zaidi kuliko kutenda, kutoaminiwa hususani kwenye kukopeshwa na suala la utunzaji wa fedha.
“Kujitambua ni lazima uangalie upungufu ulionao, uweze kujiboresha wewe mwenyewe na mbinu gani uweke, utatoka katika biashara ya kwanza , unaenda ya pili bila mafanikio yoyote,” amesema Asha.
Akieleza malengo ya mkutano huo, Mkuu wa Programu ya utafiti na Uchambuzi wa TGNP, Catherine Kasimbazi, amesema wamewaleta wanawake kutoka vituo vya maarifa na taarifa kupata elimu zaidi ya ujasiriamali.
“Kwa kuwa Stanbic wamejikita katika kuwezesha wanawake kiuchumi, tumeona ni vizuri pia wakiwa na upeo mkubwa wa kukuza biashara zao badala ya kufikiria kufanya biashara kwa ajili tu ya kupata hela ya kula.
Kai Mollel, wa Kitengo cha Kukuza Biashara benki ya Stanbic kutoka wameamua kusherehekea siku ya wanawake kutengeneza jukwaa la mazungumzo yanayolenga kukuwa kwa mwanamke kama yeye, kiongozi, mmiliki na mfanyabiashara.
“Sisi malengo yetu makubwa ni kuhakikisha tunamjenga mjasiriamali, mfanyabiashara, mbunifu na ifike mahali akue yeye na jamii yake pia.
Pia katika kukua kwake huko aweze kubeba wengine kwa njia ya kuzalisha ajira, kujikuza mwenyewe na jamii inayomzunguka,” amesema Kai.
Hata hivyo moja ya changamoto ambazo wameziona kwa wanawake katika biashara amesema na kuwa na ujuzi mdogo, namna ya kupata masoko au kuyafikia na mtaji na tatizo jingine ni wanawake kwenye biashara kwenda mmojammoja badala ya kushirikiana na wenzao .
Mmoja wa washiriki, kutokea Gongo la mboto Meshy Moses, amesema mafunzo hayo yamekuwa na manufaa kwao kwani biashara pia inahitaji uwe sawa katika afya ya akili, ambapo ni moja ya mada iliyoongelewa katika mkutano huo.
Jingine lililomfurahisha, Meshy amesema kuwepo kwa watu wa kuwafuatilia katika biashara zao ambapo ameeleza kuwa itasaidia kuwaendeleza pale wanapokwama.
Dynes Elisa kutoka Kata ya Saranga, amesema alichojifunza katika mkutano huo ni kuepuka kukurupuka katika kuanzisha bishara kwa kuwa imekuwa moja ya sababu ya watu kuishia katikati…
“Watu wengi tumeshindwa kufanikiwa kwa kuwa tunafanya biashara kwa kukurupuka, hatufanyi matumizi na mapato na hivyo kuishia njiani”