Waislamu Uhispania wahuisha mila ya karne 5 zilizopita ya Andalusia ya kwenda Hija kwa farasi

Marafiki watatu kutoka Uhispania wameamua kutumia usafiri wa farasi katika safari yao ya kuelekea Makka, Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija yao kwa madhumuni ya kuhuisha mila na desturi ya tangu miaka 500 nyuma wa Waislamu wa Andalusia ya wakati huo.