
Waasi wa Houthi nchini Yemen wamedai kufanya shambulio la nne ndani ya masaa 72 dhidi ya meli ya kivita ya Marekani inayobeba ndege za kivita za marekani USS Harry Truman katika Bahari Nyekundu, kujibu mashambulio ya Marekani dhidi ya nchi hiyo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Wahouthi “wamegundua harakati za kijeshi zenye uhasama katika Bahari Nyekundu kwa nia ya kuanzisha mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya nchi yetu,” msemaji wao aliandika kwenye Telegram.
Katika kujibu, ameongeza, waasi wamerusha makombora ya cruise na drone kadhaa dhidi ya meli ya kivita ya Marekani inayobeba ndege za kivita za marekani USS Harry Truman na meli nyingine, “hali ambayo imesaidia kuzuia na kushindwa kwa shambulio hili.”
Vyombo vya habari vya Houthi vimeripoti mapema Jumatano kwamba mashambulizi mapya ya Marekani yalilenga miji kadhaa chini ya udhibiti wa waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran, siku chache baada ya mashambulizi ya Marekani na kuua watu 53, kulingana na waasi wa Houthi.
Kulingana na shirika la habari la Saba na kituo cha televisheni cha Al Massira, “mgomo wa mashambulizi ya uvamizi wa Marekani” yalilenga jimbo la Saada (kaskazini). Walioshuhudia wameliambia shirika la habari la AFP kuwa mashambulizi matatu yalipiga eneo hilo. Baadaye, Televisheni ya Al Massira imeripoti mashambulio mengine manne kwenye eneo jingine la Saada, ngome ya Wahouthi.
Mashambulizi mengine “yalilenga Buhais, katika wilaya ya Medi, mkoa wa Hajjah” (kaskazini-magharibi), pamoja na “jengo la klabu ya al-Ahly katika eneo la Mina”, katika mkoa wa Hodeida (magharibi) na maeneo yaliyo mashariki mwa mji wa bandari wenye jina moja, kulingana na chanzo hicho.