Wahamiaji Elfu tisa walifariki mwaka uliopita wakijaribu kwenda Ulaya

Wahamiaji karibu Elfu tisa, walipoteza maisha mwaka uliopita, wakitumia usafiri wa majini kujaribu kufika barani Ulaya, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa, unasema kilichotokea mwaka 2024 ni janga, lisilokubalika, ambalo lingeweza kuzuiwa.

Wahamiaji wapatao, 8,938 waliuawa, ikiwa ni mwaka wa tano mfululizo kwa dunia kushuhudia maafa makubwa ya watu, wanaotoka katika nchi zao hasa barani Afrika, wakilenga kufika Ulaya ili kutafuta ajira.

Ugochi Daniels, Naibu Mkurugenzi wa Shririka la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, anasema kinachoshuhudiwa hakikubaliki, na huenda idadi ya vifo ni kubwa kwa sababu, watu wengine wanaopoteza maisha hawaripotiwi.

Bara la Asia, liliongoza kwa watu walipoteza maisha, ikifuatwa na Afrika na Ulaya. Watu 2,452 waliripotiwa kupoteza maisha baada ya boti walizokuwa wanasafiri kufika bara Ulaya, kuzama kaika Bahari ya Mediterenian.

Takwimu kutoka bara la America, hazifahamika vema lakini Umoja wa Mataifa unasema, watu zaidi ya Elfu moja na mia mbili walipoteza maisha, wakijaribu kufika nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *