Wahamiaji 20 wa Ethiopia wafa maji baada ya mashua yao kupinduka nchini Yemen

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuwa, wahamiaji 20 wa Ethiopia, wakiwemo wanawake tisa na wanaume 11, wamekufa maji wakati mashua yao ilipopinduka katika pwani ya kusini mwa Yemen, mwishoni mwa juma.