Wafanyakazi wa shirika la kiutu la GHF washambuliwa Gaza

Kulingana na shirika la GHF linaloungwa mkono na Marekani na Israel, timu ya wafanyakazi wake ilikuwa ikielekea kwenye kituo cha ugawaji wa chakula katika mji wa Khan Younis kusini mwa Gaza Jumatano jioni waliposhambuliwa.

Shirikahilo limeeleza kuwa watu kadhaa walijeruhiwa na huenda baadhi ya wafanyakazi wamechukuliwa mateka, likiongeza kuwa bado linakusanya taarifa za kina. Israel tayari imelishutumu kundi la Hamas kwamba “linaendeleza mateso huko Gaza” baada ya taarifa hizo.

Mpango wa kusitisha mapigano Gaza waafikiwa

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya nje wa Sweden Maria Malmer Stenergard amesema kitendo cha Israel kuzuia misaada ya kiutu kuingia Gaza na kuvilenga vituo vya usambazaji wa chakula, kinasababisha raia kufa na njaa, akiongeza kuwa suala la “kutumia njaa kama nyenzo ya vita ni uhalifu wa kivita.”

Mapema mwezi huu Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk alisema kwamba mashambulizi mabaya dhidi ya raia karibu na vituo vya kugawa misaada katika Ukanda wa Gaza yanachukuliwa kuwa “uhalifu wa kivita” huku mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu ikiwemo lile la Amnesty International yakishutumu Israel kwa mauaji ya kimbari huku nchi hiyo ikilikataa vikali neno hilo. Jeshi la Israel lauwa Wapalestina 60 karibu na kituo cha misaada.

Azimio la kushinikiza kukomeshwa vita

Nalo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura Alhamisi kuhusu azimio la kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano huko Gaza, kuachiliwa kwa mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas, na kufunguliwa kwa vivuko vyote vya mpaka vya Israel kwa ajili ya kupeleka chakula na misaada mingine inayohitajika sana. Azimio hilo, lililoandaliwa na Uhispania, “linalaani vikali matumizi yoyote ya njaa ya raia kama njia ya vita,” kama anavyoeleza waziri wake wa mambo ya nje Jose Mauel Albares.

“Tunachotaka ni kwamba nchi zote katika sayari hii zinapaswa kukemea vizuizi visivyo vya kibinadamu ambavyo Israel imeweka Ukanda wa Gaza, kuzuia misaada ya kibinadamu, kuzuia chakula, kuzuia madawa. Kwamba sisi sote tuungane kukemea vita ambayo haina lengo kubwa na kuigeuza Gaza ieneo la makaburi.”

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu bungeni
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Ohad Zwigenberg/AP Photo/picture alliance

Na huko Israel kwenyewe serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu imenusurika katika jaribio la upinzani la kulivunja bunge siku ya Alhamisi, huku wabunge wakiukataa mswada ambao ungefungua njia ya kufanyika uchaguzi wa mapema. Kati ya wabunge 120 katika bunge la Israel Knesset, wabunge 61 walipiga kura ya hapana huku 53 wakiunga mkono.

Upinzani ulikuwa umewasilisha mswada huo ukitarajia kushinikiza uchaguzi wa mapema kwa kuungwa mkono na vyama vya Kiorthodox katika muungano tawala vilivyokasirishwa na suala tata la kuondolewa kwa kinga ya wayahudi wa dhehebu hilo kutumikia jeshini. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *