
Jermaine Jenas, mchezaji wa zamani wa soka ambaye ni mtangazaji katika kipindi cha The One Show na kuonekana kwenye Match of the Day kwa BBC, amefutwa kazi na shirika hilo kufuatia malalamiko kuhusu tabia yake kazini.
Jenas mwenye umri wa miaka 41, ameondolewa kutangaza kwenye vipindi viwili muhimu.
BBC News inaelewa kuwa mkataba wake ulikatishwa wiki hii kwa sababu ya masuala yanayodaiwa kuhusiana na tabia kazini.
Akijibu habari hizo, Jenas alisema kuna “pande mbili kwa kila habari” lakini atawaacha “wanasheria wake washughulikie suala hilo”.
Madai hayo yanahusisha mawasiliano ya kidijitali kama vile maandishi, ambayo yalitolewa na shirika hilo wiki chache zilizopita.
Katika mahojiano na radio talkSport, alisema mara kwa mara “Siwezi kuzungumza juu yake” alipoulizwa juu ya madai hayo.
“Mimi, kama unavyoona, sifurahii suala hilo,” aliambia kituo hicho.Alipoulizwa kama alishangazwa na malalamiko yoyote dhidi yake, Jenas alisema tena: “Siwezi kuzungumza kwa sasa.”
“Lazima niiachie timu ya wanasheria kwa sasa ambao ni, ndio, nadhani wanashughulikia hali hiyo,” alisema.”Hii ni…, ni ngumu, unajua. Lakini sina budi kuwasikiliza mawakili wangu.
“Msemaji wa BBC alisema: “Tunaweza kuthibitisha Jermaine Jenas si sehemu yetu ya watangazaji.”
Alikuwa hewani mara ya mwisho kwa shirika hilo mapema wakati wa msimu wa kusi.
Jenas, ambaye ameoa na ana watoto wanne, alipata mshahara wa kati ya £190,000 – £194,999 katika idhaa BBC kwa kazi yake ya Kombe la FA, Mechi Bora ya Siku na Kombe la Dunia.