Wafanyabiashara wa Rwanda wana hofu kufuatia mzozo wa DR Congo

Wasafirishaji wa malori na wasafirishaji wa mizigo kutoka Rwanda wanasema wanapitia wakati mgumu kutokana na mzozo huo katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakilazimika kukabiliana na mashambulizi ya wakaazi wenye hasira ambao ni raia wa Kogo wanaoshtumu kwamba Rwanda inawaunga mkono wapiganaji wa M23.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Wengi wa madereva wa malori hayo ya mizigo wanayoichukua katika bandari ya Dar es Salaam, Tanzania wanaeleza kwamba wanakumbana wanapitia wakati mgumu wanaposafirisha mizigo hiyo nchini DRC.

Wasafirishaji wa mizigo wa Rwanda sasa wana hofu kwamba mzozo unaoendelea mashariki mwa Kongo utaendelea kuziathiri biashara zao za usafirishaji.

Olivier Munyemana, dereva wa lori kutoka Rwanda, anaifahamu kwa moyo barabara kutoka bandari ya Bahari ya Hindi ya Dar es Salaam hadi DRC, akiwa ameiendesha kwa miaka minane.

Lakini wakati mapigano yakiongezeka nchini DRC katika miezi ya hivi karibuni, huku kundi la waasi wa M23 linaloungwa mkono na Rwanda likiteka maeneo makubwa ya mashariki, ikiwa ni pamoja na miji ya mpakani ya Goma na Bukavu, amekuwa akiogopa kupita maeneo hayo.

Anasema madereva wa lori wanashambuliwa na wakaazi wenye hasira kutokana na kuhusika kwa Rwanda katika mzozo huo.

“Siwezi kuhatarisha maisha yangu au kupoteza lori langu,” ameliambia shirika la habari la  AFP. “Tumekuwa na visa vya malori kuchomwa moto na madereva kushambuliwa.”

Rwanda inabaini kwamba M23 kudhibiti eneo la mashariki mwa DRC ni muhimu ili kutokomeza kundi la wanamgambo wa Rwanda ambao awali liliundwa na wale waliofanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 na ambalo linatishia kushambulia mipaka yake.

DRC inasema Rwanda inatafuta mabadiliko ya utawala na udhibiti wa utajiri mkubwa wa madini mashariki.

Makampuni pia yanapoteza wateja baada ya makampuni ya ujenzi huko Bukavu na Goma kulengwa wakati wa machafuko au kukimbia ghasia, amesema Davis Twahirwa, meneja mauzo wa Cimerwa, kampuni nyingine ya saruji ya Rwanda, ambayo kwa kawaida imekuwa ikiuza theluthi moja ya uzalishaji wake nchini DRC.

“Baadhi ya wateja wangu wamepoteza mamilioni ya fedha,” ameliambia shirika la habari la AFP. “Mmoja wao alipoteza lori mbili mpya kabisa huko Goma… inaonekana ziliibwa na vikosi vya serikali, na bohari zake pia ziliporwa.”

Amesema benki katika maeneo yanayodhibitiwa na M23 zimefungwa na serikali ya Kongo, na hivyo kufanya kuwa vigumu kupata dola, na wafanyabiashara wengi wanahofia kuwa serikali itawaadhibu wafanyabiashara ambao wataanza tena shughuli zao chini ya mwavuli wa M23.

Ameongeza, hata hivyo, kwamba hali ya utulivu imeanza kurejea kwa sasa kwa vile kundi hilo limekuwa likiimarisha udhibiti wake katika eneo hilo.

“Hali ya kawaida inarejea na tumeanza kuuza tena katika masoko yote mawili, haswa huko Goma, Bukavu pia hali ya utulivu inarudi hatu kwa hatua na tunatumai kuanza kazi kikamilifu katikati mwa mwezi Machi,” Twahirwa amesema.

Kwa vile mahitaji yameongezeka katika nchi za bara la Afrika Mashariki katika muongo mmoja uliopita, Wanyarwanda wengi wamewekeza katika malori ya kufanya safari kutoka bandari za pwani za Mombasa na Dar es Salaam.

Mahitaji yalipoongezeka katika nchi za bara la Afrika Mashariki katika muongo uliopita, Wanyarwanda wengi waliwekeza kwenye malori ili kusafirisha mizigo kutoka bandari za pwani za Mombasa na Dar es Salaam.