Wakuu wa nchi na serikali za mataifa ya Afrika siku ya Jumamosi, watapiga kura kumchagua Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika, kumrithi Moussa Faki.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mwenyekiti huyo mpya anatarajiwa kutokea kwenya mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki.
Wagombea watatu, watakaotoana jasho, ni Raila Odinga kutoka nchini Kenya, Mahamoud Ali Youssouf kutoka Djibouti na Richard Randriamandrato kutoka nchini Madagascar.

Mahamoud Ali Youssouf mwene umri wa miaka, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje nchini Djibouti atakuwa analeta maswala ya diplomasia na pia uzoevu wake kuhusu utendakazi wa taasisi za Umoja wa Afrika.
Aidha akiwa anazungumza lugha za kiingereza, Kiarabu na Kifaransa anatazamia kuitumia tunu hiyo kuishawishi nchi zinazozungumza kiangereza kifaransa na muungano wa nchi za Kiarabu.

Kwa upande mwingine Raila Odinga, Waziri mkuu wa zamani nchini Kenya mwanasiasa wa upinzani mkongwe naye analeta msisimiko wa siasa za Afrika na wito wa Afrika kusimama na kuwa na sauti ya pamoja.
Na mgombea wa tatu Richard Randriamandrato kutoka Madagascar, alikuwa ni waziri wa zamani wa uchumi na fedha nchini mwake.

Aliwahi kufanya kazi na shirika la kimataifa la leba na muungano wa COMESA.
Carol Korir Addis Ababa