Wafadhili waahidi dola bilioni 8 kusambaza umeme Afrika

Benki ya Maendeleo ya Afrika na wakopeshaji wengine wa kimataifa wameahidi zaidi ya dola bilioni 8 zitakazotumika kwenye mkakati wa kuwawezesha Waafrika milioni 300 kupata umeme katika kipindi cha miaka sita ijayo. Mpango huo unaoitwa “Mission 300” uliozinduliwa na Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika mwezi Aprili, unakadiriwa kugharimu dola bilioni 90.