Wadau waombwa kusapoti Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi wetu

Wadau mbalimbali na Watanzania wameobwa kujitokeza kwa wingi kudhamini Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu litakalofanyika katika mikoa 26 nchini

Hayo amebainisha hii leo April 2, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama amesema tamasha hilo halitakuwa na kingilo ili kila mtanzania aweze kushiriki kwenye kuliombea taifa huku maandilizi yakiwa yanaendele vizuri

Msama ameongeza kuwa tamasha litaanzia katika mkoa wa Dar es salaam na kwenda mikoa mingne na limehusisha Wachungaji, Maskofu wa mikoa mbalimbali katika kuhakikisha wanaombea amani kulekea uchaguzi Mkuu.

Aidha amesema waimbaji mbalimbali wakubwa kutoka nje ya nchi na Ndani ya nchi watakuwepo kwenye tamasha la Kuombea Uchaguzi.

” Tutatangaza tarehe na eneo ambalo tamasha hili litafanyika hivi karibuni kwa mkoa wa Dar es salaam ambapo tamasha hili ndipo litakapo anzia” amesena Masama

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Barazaa Makanisa ya Kipenteksote Mkoa wa Dar es salaam, Mch Emmanuel Mwasota amesema tamasha hilo lipo kwajili ya Maombi ya Kuombea uchaguzi Mkuu kwa kuungana kwa pamoja kwa waumi wote wa madhehebu yote kuiombea nchi yetu, viongozi , wabunge, madiwa na Rais wetu ili chaguzi uweze kupita kwa amani

“Sisi tumesema ya kwamba tutashikama kwa pamoja na taarifa hizi zinaenda kila mahali kwa makanisa, wachungaji, maskofu na waubiri wa aina mbalimbali tutakuwa kwa Pamoja kwaajili ya kuhakikisha tunaombes nchi yetu ipite salama kwenye uchaguzi utakaofanyika mwaka huu”

Ameongeza kuwa uchaguzi unaweza kusabisha nchi inaweza ikapasuka kama raia wake wasipokuwa wazalendo hasa kwa upande wa amani kwajili ya kuombea nchi na viongozi wetu ambao wanatuongoza katika maswala ya nchi yetu na sisi tunahitaji amani na maombi ili tuweze kuvuka kwenye uchaguzi kwa amani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *