Wachumi na watafiti wa masuala ya kijamii wamesema Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2025/2026 inatarajiwa kuelekezwa zaidi katika kuboresha uchumi wa wananchi mmoja mmoja, hasa baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya kimkakati iliyotumia fedha nyingi katika miaka ya nyuma.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuwasilisha bajeti hiyo bungeni kesho, Juni 12,2025 huku macho na masikio ya Watanzania yakielekezwa Dodoma. Wananchi nao wameeleza matarajio yao wakitamani kusikia ahueni katika maisha ya kila siku, fursa za ajira na unafuu wa bidhaa muhimu.
#azamnewsupdates
✍️Tumie Omar
Mhariri| @official_jennifersumi