
Licha ya chama cha Waziri Mkuu Albin Kurti cha VV kushinda uchaguzi wa Februari 9 kwa kuchukua viti 48 kati ya 120 bya bunge, hakikutimiza idadi iliyohitajika ya kukiwezesha kuunda serikali.
Kikisisitiza kuteuliwa kwa mgombea wake na waziri wa sheria wa zamani Albulena Haxhiu katika nafasi hiyo ya uspika, chama hicho cha VV bado hakijapata kura 61 kumuezesha Haxhiu kuchukua nafasi hiyo.
Kikao hicho kwa sasa kimeahirishwa hadi siku ya Ijumaa. Kulingana na kanuni za bunge, bunge haliwezi kuapishwa na kuwa halali bila spika, na bila bunge hilo jipya serikali mpya pia haiwezi kuundwa hatua inayosababisha mkwamo katika uongozi wa nchi.