Waasi wa M23 waingia Bukavu baada ya kutwaa uwanja wa ndege

Waasi wa M23 wametangaza habari ya kuingia katika jiji la Bukavu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. siku ya Ijumaa, kiongozi wa waasi aliliambia shirika la habari la Reuters, huku wakaazi wakiripoti kuwaona wanamgambo hao katika mitaa ya wilaya ya kaskazini.