Waasi wa Kongo wanapanga kusonga mbele hadi Kinshasa, Rais Tshisekedi atoa wito wa kujitayarisha

Waasi wa kundi la M23 la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linaloungwa mkono na Rwanda, ambalo limeteka mji mkubwa zaidi mashariki mwa nchi hiyo, Goma, wametangaza nia yao ya kupeleka vita katika mji mkuu, Kinshasa, huku Rais Félix Tshisekedi akitoa wito wa kuandaliwa jeshi kubwa kukabiliana na mashambulizi hayo.