Waasi wa DRC watangaza kuwa tayari kwa usitishaji mapigano

Muungano wa waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Alliance Fleuve Congo (AFC), unaojumuisha waasi wa M23, umetangaza kuwa tayari kushiriki mazungumzo na serikali ili kusitisha mara moja mapigano mashariki mwa nchi, msemaji wa kundi hilo amesema.