Vyombo vya habari Kenya vyazungumzia athari za ushindi wa Odinga kama mkuu wa Kamisheni ya AU

Vyombo vya habari vya Kenya vimechapisha ripoti kuhusu athari za matokeo ya ushindi wa mgombea wa nchi hiyo, Raila Odinga, katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, unaotarajiwa kufanyika wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Afrika mjini Addis Ababa wiki ijayo, katika siasa za ndani nchini Kenya.