Vyanzo vya jeshi Sudan: Dagalo anatekeleza Mpango B katika vita vya ndani

Vyanzo vya kijeshi katika Wizara ya Ulinzi ya Sudan vimefichua kwamba Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) hivi sasa vinatekeleza Mpango B (mpango mbadala) ambao kamanda wake, Mohamed Hamdan Dagalo “Hemedti”, alitishia kuutekeleza baada ya kushindwa kunyakua madaraka.