Vyama vya ACT Wazalendo na CUF Zanzibar vinatarajia kufanya uchaguzi wa kura ya maoni ndani ya vyama hivyo ili kupata wagombea wa nafasi mbalimbali kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ACT Wazalendo, Mhene Rashid, amesema zaidi ya wanachama 1,000 wamejitokeza kuwania nafasi hizo.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Ali Juma Khamis, amethibitisha ushiriki wa chama hicho katika uchaguzi, huku wakisisitiza msimamo wao wa kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
#azamnewsupdates
Mhariri| @official_jennifersumi