
Majadiliano ya kitaifa nchini DRC yalizinduliwa Jumatatu ya wiki hii jijini Kinshasa, yakilenga kupata mwafaka kuelekea kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kiataifa.Hata hivyo vyama kadhaa vya upinzani vimesusia kushiriki.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Waziri Mkuu Judith Suminwa alikuwa wa kwanza kupokelewa, Augustin Kabuya Katibu Mkuu wa chama kilicho madarakani na baadae Spika wa bunge la Senete Sama Lukonde ambaye alipokelewa kama mjumbe wa viongozi wa vyama ambavyo vinamuunga mkono chama cha rais Tshisekedi Union sacrée.
‘‘Tulikuja kuthibitisha kanuni ya umoja, lakini zaidi ya hapo, kushiriki katika wazo hili la Raïs wa Jamhuri, lakini tulisema limepaswa kuzingatia heshima ya katiba, heshima na utaratibu za taasisi zilizowekwa tayari.’’
Vyama vya kisiasa kadhaa za upinzani kama vile FCC ya Joseph Kabila, Ensemble ya Katumbi, Envol ya Delly Sesanga, Lamuka chake Martin Fayulu na LGD chake Matata Ponyo vilisusia mpango huu.
Promesse Matofali ni kiongozi wa chama cha Katumbi jimboni Kivu kaskazini.
‘‘Kama ni kugawana viti hao wafanye kule ila sisi lakini hilo halitamaliza mzozo ndani ya nchi.” alisema Promesse Matofali ni kyongozi wa chama cha Katumbi jimboni Kivu kaskazini.
Mbele ya wanachama wa Union sacrée, Mnamo Februari 22, Rais Tshisekedi, alitangaza mazungumzo ya kitaifa, ili kuunda serikali ya pamoja kwa lengo la kumaliza migogoro za ndani na vitisho toka nje haswa mashariki mwa DRC.
Freddy Tendilonge/ Kinshasa RFI kiswahili.