
Wakati wajumbe wa Ufaransa na Uingereza walipokuwa kyiv kukutana na Rais Volodymyr Zelensky siku ya Ijumaa, Aprili 4, kujadili uwezekano wa kuwepo kwa wanajeshi wa kulinda amani wa kigeni katika ardhi ya Ukraine, Urusi inaendelea kuishambulia Ukraine kila siku. Ndege zisizo na rubani zilizinduliwa tena usiku wa Aprili 4 kuamkia Aprili 5 katika maeneo kadhaa ya nchi, wakati siku moja mapema, jiji la Kryvyi Rig lilipigwa tena na kombora la balestiki la Urusi.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Katika Kryvyi Rig, mji alikozaliwa Rais Zelensky, idadi ya vifo kutokana na shambulio la Urusi mnamo Aprili 4 ilikuwa kubwa: watu kumi na wanane waliuawa, ikiwa ni pamoja na watoto tisa, na karibu sitini walijeruhiwa wakati kombora la balistiki, kombora la Iskander, kulingana na Kyiv, lilipiga eneo la makazi, anaandika mwandishi wetu huko Kyiv, Emmanuelle Chaze. Urusi imejibu kwamba lilikuwa “shambulio la usahihi na kombora la vilipuzi kwenye mgahawa” katika jiji “ambapo makamanda na wakufunzi wa nchi za Magharibi wamekuwa wakikutana.” Hata hivyo, picha zinaonyesha shambulio kwenye eneo la makazi, karibu na uwanja wa michezo wa watoto.
Mji wa Kryvyi Rig ambao uko umbali wa kilomita 80 kutoka mstari wa mbele, umekuwa ukilengwa mara kwa mara na mashambulizi ya anga tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi Februari 2022. Takriban watu 600,000 waliishi hapo kabla ya vita.
Miili yatapakaa barabarani
Picha zilizotolewa na idara ya huduma za dharura ya Ukraine zinaonyesha watu kadhaa wameuawa, ikiwa ni pamoja na mmoja amelala mbele ya bembea, shirika la habari la AFP linaripoti. Video zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii, ambazo hazikuweza kuthibitishwa, zimeonyesha miili ikiwa imetapakaa barabarani na moshi mwingi ukipanda angani. Picha zingine zinaonyesha gari likiwaka moto na watu wakipiga kelele.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amejibu vikali akisema: “Warusi wanafanya mashambulizi kila siku. Watu wanakufa kila siku. Kuna sababu moja tu inayoendelea: Urusi haitaki kusitishwa kwa mapigano, na Ukraine na ulimwengu wote wanaona.” Mashambulio hayo yanakuja wakati wajumbe wakiongozwa na wakuu wa majeshi wa Ufaransa na Uingereza wako mjini Kyiv kujadili uwezekano wa kuwepo kwa vikosi vya kigeni vya kulinda amani katika ardhi ya Ukraine.
“Usaidizi kwa wakati”
Lengo la ziara hii ya pamoja ilikuwa “kubadilishana mahitaji na malengo ya kijeshi ya Ukraine ili kulisaidia kwa muda mrefu katika ujenzi na maendeleo ya mtindo wake,” Mkuu wa majeshi ya Ufaransa amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari. Kwa hiyo lilikuwa ni suala la kuhakikisha “kudumisha msaada uliodhamiriwa kwa jeshi la Ukraine, kuwezesha kuendelea na mapambano” dhidi ya Urusi, kulingana na Jenerali Burkhard, na pia kufafanua “mkakati wa muda mrefu wa ujenzi na mabadiliko ya mtindo wa jeshi la Ukraine, dhamana ya msingi ya usalama wa nchi hii.”
Paris na London, AFP pia inaandika, zinajitahidi kujenga muungano wa nchi zilizo tayari kupima juu ya mazungumzo yaliyoanzishwa na Washington na Moscow ili kumaliza mzozo huo na kuanzisha “operesheni za uhakikisho” ili kuizuia Urusi kuanza tena uhasama.
Wakati huo huo, mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi ilinasa na kuharibu ndege zisizo na rubani 49 zilizorushwa na Ukraine usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Moscow pia imetangaza.