
Mashambulizi ya makombora ya Urusi na ndege zisizo na rubani yaliyoendeshwa usiku wa Jumatano 23 kuamkia Alhamisi 24 Aprili yamesababisha vifo vya watu wanane na zaidi ya 70 kujeruhiwa huko Kyiv, mji mkuu wa Ukraine, kulingana na ripoti ya hivi karibuni, idara ya huduma za dharura imesema. Watoto sita wako kwenye orodha ya waliojeruhiwa. Kwa upande wake, jeshi la Urusi linasema limelenga kiwanda cha jeshi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
“Shambulio la Urusi limesababisha uharibifu mkubwa.” “Msako unaendelea kuwatafuta watu chini ya vifusi,” idara ya huduma za dharura imesema kwenye Telegram. Jengo la makazi limeharibiwa katika wilaya ya Sviatoshynskyi magharibi mwa mji mkuu wa Ukraine.
Operesheni za utafutaji zilikuwa zikiendelea katika maeneo kumi na tatu jijini Kyiv na zaidi ya visa vya moto arobaini vimeripotiwa, kulingana na idara ya huduma za dharura. “Simu za rununu zimesikika zikiita chini ya vifusi. Msako utaendelea hadi itakapobainika kuwa wamepata watu wote walio chini ya vifusi,” idara hiyo imeongeza.
Arifa za mashambulizi ya anga zimesikika kwa saa sita huko Kyiv. Kharkiv, mji wa pili kwa ukubwa mashariki mwa Ukraine, ulikumbwa na mawimbi mawili ya mashambulizi ya makombora ya Urusi usiku kucha, na kuwajeruhi watu wawili na kuvunja madirisha, Meya Ihor Terekhov ameandika kwenye Telegram.
Uharibifu pia ulionekana katika mkoa wa Zhytomyr, magharibi mwa Kyiv, ambapo vikosi vya Urusi vimeanzisha shambulio jipya kwa timu za uokoaji zinazofanya kazi ya kuzima moto, na kumjeruhi mfanyakazi mmoja, shirika la habari la REUTERS limeripoti. Kampuni ya reli ya Ukrzaliznytsia pia imeripoti kuwa wafanyikazi wake wawili wamejeruhiwa katika shambulio dhidi ya miundombinu yake. Katika mikoa ya Kyiv na Kharkiv, makombora yameharibu njia za reli na majengo ya kiutawala na kiufundi, lakini treni zilikuwa zikitembea kawaida.
Tuhuma za Donald Trump
Shambulio hilo linafuatia maoni ya Donald Trump, ambaye aliishutumu Ukraine kwa kutotaka amani kwa kukataa kutambua unyakuzi wa Crimea. Volodymyr Zelensky hakuchelewa kujibu, akikumbusha Washington juu ya taarifa zake za mwaka 2018 za kupinga unyakuzi wa Moscow wa eneo hilo.
Kufuatia mkutano wa London na Marekani, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, Volodymyr Zelensky amekaribisha uzinduzi wa diplomasia. Lakini ameambatanisha kwenye tweet ujumbe wake wa kwenye ukurasa wake wa Twitter taarifa iliyotolewa na Marekani mwaka 2018, wakati wa muhula wa kwanza wa Donald Trump, ikibainisha kwamba Marekani haitakubali Moscow kunyakua Crimea.
Majibu kwa saa 48 zilizopita ambapo Donald Trump na washirika wake wa karibu wameishutumu Ukraine kwa kutocheza mchezo huo na kutotaka amani kwa kuonyesha kwamba anakataa kutambua kunyakuliwa kwa Crimea, akisema kuwa “imepotea” kwa miaka mingi. Hata hivyo, Volodymyr Zelensky amerejelea msimamo wake mara kwa mara: hakuna suala la kuanzisha majadiliano na Urusi bila usitishaji wa mapigano, anaripoti mwandishi wetu wa Kyiv, Cerise Sudry-Le Dû.
Siku ya Alhamisi Aprili 24 rais wa Ukraine ametangaza kwamba anakatisha ziara yake ya sasa nchini Afrika Kusini ili kurejea Ukraine. Ameshutumu shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine ambalo liliua takriban watu tisa usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu, Kyiv, na kuitaka Urusi “ikomeshe mara moja” mashambulio yake.
“Imepita siku 44 tangu Ukraine ikubali kusitisha mapigano kabisa na kusitisha mashambulizi. “Na kwa muda wa siku 44 Urusi imeendelea kuwaua watu wetu,” kiongozi wa Ukraine amejibu katika ujumbe wake kwenye X, akiongeza kwamba “mashambulizi yanapaswa kukomeshwa mara moja na bila masharti.”