Vita vya maneno vyaibuka kati ya Ukraine na Urusi kabla ya mazungumzo Istanbul

Wajumbe wa Urusi na Ukraine wanatarajiwa kukutana leo Alhamisi, Mei 15, “katika sehemu ya pili ya siku” huko Istanbul ili kujadiliana na labda kujadili mwisho wa vita nchini Ukraine. Kwa sasa, pande hizo mbili zinapaza sauti. Uturuki, hata hivyo, inasema ina “sababu za kukuwa na matumaini.”

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameuita ujumbe uliotumwa na Moscow kuwa “bandia” wakati Rais wa Urusi Vladimir Putin hakuhudhuria mazugumzo hayo. Moscow imejibu kwa kumwita “muigizaji mcheshi” na kiongozi “anayetia huruma”, na kutilia shaka matokeo ya mazungumzo kabla hata hayajaanza. Na matumaini ya kufikia hatua kubwa katika mazungumzo haya, ya kwanza katika miaka mitatu, bado ni kitendawili.

Kwa hakika, ugumu wa kufikia usitishwaji mapigano ni kwamba Kyiv na Moscow hazina madai sawa juu ya suala muhimu, yaani makubaliano ya amani yanayowezekana. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Ulaya wanaitaka Urusi kukubali kusitisha mapigano kabla ya mazungumzo. Vladimir Putin, kwa upande wake, anataka majadiliano juu ya “sababu kuu za vita” kabla ya uwezekano wa kusitisha mapigano.

Madai ya upande mmoja yajikuta katika upinzani na madai ya upande mwingine

Hizi “sababu za mizizi”, zilizotajwa na Moscow, pia husababisha pointi nyingine za kutokubaliana. Tangu mwanzo wa uvamizi, Vladimir Putin amedumisha matakwa ya hali ya juu. Anasisitiza kwamba mchakato wa suluhu lazima ushughulikie “sababu kuu” za mzozo, kwanza kabisa nia ya Ukraine ya kujiunga na NATO, na pia anadai kuunganishwa kwa mikoa minne ya kusini na mashariki mwa Ukraine ambayo ambayo Urusi inadhibiti kwa sehemu (Donetsk, Lugansk, Kherson, Zaporizhzhia) na peninsula ya Crimea, mnamo mwaka 2014.

Ukraine inaendelea kudai kuondolewa kabisa kwa wanajeshi wote wa Urusi kutoka katika eneo lake. Na Volodymyr Zelensky anasisitiza wazi kwamba kyiv haitatoa Crimea, kwa sababu Katiba ya Ukraine inasema kuwa ni sehemu ya eneo lake. Kwa upana zaidi, Volodymyr Zelensky anatoa wito kwa washirika wake kutoa “dhamana ya usalama” kwa Ukraine ili kuzuia Urusi kuivamia tena baada ya makubaliano ya amani kufikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *