
Wawakilishi kutoka China na Marekani wanaketi kwenye meza moja ya mazungumzo siku ya Jumamosi, Mei 10, na Jumapili, Mei 11, huko Geneva, nchini Uswisi, kujaribu kutafuta suluhu la vita vyao vya kibiashara. Siku moja kabla, Donald Trump aliweka misingi ya mazungumzo kwa kupendekeza kupunguzwa kwa ushuru wa forodha kwa bidhaa za China hadi 80%.
Imechapishwa:
Dakika 3
Matangazo ya kibiashara
Tangu arejee Ikulu ya White House, Donald Trump ametoza ushuru wa ziada wa 145% kwa bidhaa kutoka China. Mazungumzo haya yanalenga kupunguza mgogoro, lakini China inataka kuonyesha kwamba inatumia ushawishi wake.
China na Marekani zimeanza mazungumzo yao rasmi ya kwanza mjini Geneva siku ya Jumamosi, Mei 10, katika jaribio la kutuliza hali katika vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Rais wa Marekani Donald Trump, kulingana na televisheni ya taifa ya China CCTV. “Mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya China na Marekani” yalianza asubuhi, CCTV imeripoti, bila kutoa maelezo ya majadiliano kati ya Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent na Makamu wa Waziri Mkuu wa China He Lifeng katika eneo lisilojulikana.
Rais wa Marekani Donald Trump alionekana kuchukua hatua kuelekea Beijing siku ya Ijumaa kwa kupendekeza kwamba anaweza kupunguza ushuru wa adhabu aliotoza yeye mwenyewe kwa bidhaa za China hadi asilimia 80, kabla ya mazungumzo yaliyokuwa yanatarajiwa nchini Uswisi. “Asilimia 80 ya ushuru kwa China inaonekana kuwa sawa!” “Inategemea na Scott B,” rais wa Marekani ameandika kwenye mtandao wake wa Truth Social, akimaanisha mtu ambaye ataongoza mazungumzo ya Washington, Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent.
Baada ya majuma kadhaa ya mvutano mkali kati ya nchi hizo mbili, Katibu wa Hazina na Mwakilishi wa Biashara Jamieson Greer wamepangwa kukutana na Makamu Mkuu wa China He Lifeng mwishoi mwa juma hili huko Geneva. Mahali halisi bado hapajajulikani. “Juzi (Alhamisi, Mei 8), Roho Mtakatifu alikuwa Roma. “Tunatumai sasa atashuka Geneva kwa wikendimwxishoni mwa juma hili,” amesema Rais wa Uswisi Karin Keller-Sutter, akimaanisha kuchaguliwa kwa Papa Leo XIV.
Biashara baina ya nchi mbili imesimama kivitendo
Tangu arejee Ikulu ya Marekani mwezi mwezi Januari, Donald Trump ametoza ushuru wa ziada wa 145% kwa bidhaa kutoka China, juu ya ushuru uliopo. Beijing ililipiza kisasi kwa kuweka ushuru wa 125% kwa bidhaa za Marekani. Athari: biashara ya nchi mbili imesimama kivitendo.
Kwa Waziri wa Uchumi wa Uswisi Guy Parmelin, tayari ni “mafanikio” kwamba “pande zote mbili zinazungumza kwa kila mmoja.” “Unaweza kufikiria chochote,” aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa. “Kusitishwa, kwa mfano, kwa ushuru wa forodha kwa muda wote wa majadiliano. Lakini hilo ni suala la pande zote mbili. Na hilo lingekuwa chanya, uamuzi wa dhahania kama huo ungekuwa mzuri kwa ulimwengu wote.”
Majadiliano yaliyopangwa mjini Geneva ni “hatua chanya na yenye kujenga kuelekea kupunguka kwa mgogoro,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala.
China katika nafasi ya nguvu
Kwa kujiamini kuwa mhasiriwa wa uchokozi usio wa haki, Beijing imecheza na wakati kabla ya kukubali kufanya mazungumzo. Makamu Mkuu wa China ambaye amesafiri hadi Uswizi alikuwa na shauku ya kusema kwamba majadiliano haya yalikuwa yakifanyika “kwa ombi la Marekani.”
China inajua kwamba wakati upo upande wake, kwamba Marekani inaitegemea kwa bidhaa nyingi, na kwamba hali hiyo inaweza tu kusababisha mfumuko wa bei ambao ni wenye nguvu sawa na usiopendeza, madhara ya kwanza ambayo yataonekana hivi karibuni. Hata hivyo, Beijing haiwezi kumudu kabisa kuachana na soko la Marekani, ikizingatiwa kwamba ilisafirisha bidhaa zenye thamani ya karibu dola bilioni 440 huko mwaka wa 2024 na inakabiliwa na kushuka kwa ukuaji ambao hatua za kichocheo za Chama tawala cha Kikomunisti zinajitahidi kukomesha.
Scott Besent ameonya kuwa mpango mkubwa wa biashara hautarajiwi. Hata hivyo, shinikizo linaongezeka huku muda wa mwisho wa Donald Trump wa mazungumzo kabla ya kurejeshwa kwa ushuru utamalizika tarehe 8 Julai.