Vita vya Gaza katika kitovu cha ziara ya Emmanuel Macron nchini Misri

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anafanya ziara rasmi nchini Misri leo Jumatatu, Aprili 7 na kesho Jumanne, Aprili 8. Hii ni mara ya nne kwa Rais wa Ufaransa kuzuru nchi hii ya kimkakati katika eneo hilo tangu uchaguzi wake wa kwanza mwaka wa 2017. Na wakati huu, suala moja litatawala: kusitishwa kwa mapigano huko Gaza, wakati Israel imeanzisha tena mashambulizi yake katika mji huo.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Misaada ya kibinadamu kwa Gaza hupitia mji huu wa bandari wa Sinai, kupitia kituo cha Rafah. Rais wa Ufaransa atataka kuonyesha uungaji mkono wake kwa kusitishwa kwa mapigano ardhini, kwani mashambulizi ya Israeli yameanza tena katika Ukanda wa Gaza. “Hatua kubwa ya kurudi nyuma” kulingana na mkuu wa nchi, ambaye anatarajiwa kukutana na wadau wa shirika la Hilali Nyekundu ya Misri, pamoja na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali. Hii ni njia ya kuzingatia masuala muhimu ya kibinadamu na afya, wakati raia katika Ukanda wa Gaza wako katika hali ya kukata tamaa, anakumbusha Valérie Gas, mkuu wa kitengo cha kisiasa cha RFI, kutoka mji mkuu wa Misri.

Kabla ya hapo, Emmanuel Macron, ambaye aliwasili Cairo Jumapili jioni, Aprili 6 – ambapo alizuru Jumba jipya la Makumbusho la Grand Egypt, ambalo bado halijafungua milango yake – anatarajiwa kushiriki katika mkutano wa kilele wa nchi tatu siku ya Jumatatu na Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi na Mfalme Abdullah wa Jordan, wawakilishi wa nchi mbili muhimu katika usimamizi wa mgogoro huo. Baada ya wiki kadhaa kuhusu vita vya Ukraine, Emmanuel Macron anataka kuonyesha, kwa ziara hii, kwamba anaendelea kujikita katika suala la Gaza.

Cairo inategemea uungwaji mkono wa Macron kwa mpango wake wa ujenzi wa Gaza 

Kwa mujibu wa Cairo, jambo muhimu zaidi kuhusu ziara ya Emmanuel Macron ni ziara yenyewe. Wakati hii ikiwa ni mara ya nne kwa rais wa Ufaransa kuzuru Misri, mwenzake wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, tayari ameitembelea Ufaransa mara nane, anakumbusha mwandishi wetu katika mji mkuu wa Misri, Alexandre Buccianti. Uthibitisho, kama upo unahitajika kwa Cairo, uthabiti wa uhusiano wake wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi na Paris.

Kwa kukosekana kwa mikataba yenye faida kubwa, Misri, ambayo uchumi wake unayumba, itasaini mikataba mingi ya ushirikiano na Ufaransa katika ngazi ya chuo kikuu na katika sekta ya uwekezaji wa kampuni za Ufaransa. Misri pia inaichukulia ziara ya rais wa Ufaransa kama kuunga mkono mpango wa Misri wa kuijenga upya Gaza bila ya kuwaondoa Wapalestina, kama alivyotaka Rais wa Marekani Donald Trump. Hii ndiyo sababu Emmanuel Macron alipewa nafasi nyingine ya kukutana na Mfalme wa Jordan na kutembelea El-Arish,  kilomita zisizozidi hamsini kutoka Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *