Vita Ukraine: Macron kumpokea Zelensky Jumatano jioni kwa maandalizi ya mkutano wa usalama

Rai wa Ufaransa Emmanuel Macron atampokea mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika Ikulu ya Élysée siku ya Jumatano jioni, Machi 25, ili “kutayarisha” mkutano wa kilele  wa nchi za “muungano wa walio” tayari kutoa dhamana ya usalama kwa Ukraine siku iyakayofuata huko Paris, ofisi ya rais wa Ufaransa imetangaza Jumanne, Machi 25.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Mkuu wa Nchi atasisitiza tena kwa Rais Zelensky kwamba Ufaransa itafanya muendelezo na uimarishaji wa msaada wa kijeshi na kifedha kwa Ukraine kuwa kipaumbele chake cha juu,” Ikulu ya Élysée imesema katika taarifa. Viongozi hao wawili watatoa taarifa kwa vyombo vya habari, kabla ya mkutano wa pande mbili na chakula cha jioni.

Siku ya Alhamisi asubuhi, Emmanuel Macron atafanya mkutano mpya wa kilele kuhusu “amani na usalama kwa Ukraine,” kufuatia mikutano iliyofanyika Paris na London katika wiki za hivi karibuni ili kuweka “dhamana ya usalama” kwa Kyiv kama sehemu ya uwezekano wa makubaliano ya amani ya baadaye na Urusi, ambayo Marekani ya Donald Trump inajaribu kuyakamilish.

“Mfano endelevu na a kudumu wa jeshi la Ukraine”

Toleo hili jipya linapaswa kuruhusu “kukamilika” kwa kazi ya msaada wa kijeshi wa “muda mfupi” kwa Ukraine, juu ya “mfano endelevu na wa kudumu wa jeshi la Ukraine ili kuzuia uvamizi wa Urusi” katika siku zijazo, na juu ya “dhamana ya usalama ambayo majeshi ya Ulaya yanaweza kutoa,” ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwa waajeshi kupitia ardhini nchini Ukraine, rais wa Ufaransa alisema wiki iliyopita.

Kulingana na chanzo cha kidiplomasia, zaidi ya nchi ishirini kutoka Umoja wa Ulaya na/au NATO zimealikwa siku ya Alhamisi, zikiwemo Uingereza, Canada, Norway na Uturuki.

Wakati huo huo, Emmanuel Macron anaendelea na tafakari yake ya kitaifa juu ya kuimarisha juhudi za ulinzi huko Ufaransa na Ulaya kwa nia ya Marekani ya kujiondoa. Kwa mara ya tatu katika wiki za hivi karibuni, atampokea Waziri Mkuu François Bayrou na mawaziri kadhaa Jumanne alasiri kwa mkutano wa kufanya kazi juu ya matumizi ya ziada ya kijeshi wanayoamini ni muhimu na ufadhili wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *