
Mazungumzo kuhusu kusitisha mapigano nchini Ukraine “yataanza Jumapili mjini Jeddah,” Saudi Arabia, mjumbe wa Marekani Steve Witkoff amesema siku ya Jumanne, Machi 18, baada ya mazungumzo ya simu kati ya Rais Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Kuhusiana na usitishwaji mashambulizi kwenye miundombinu ya nishati na usitishaji vita wa baharini katika Bahari Nyeusi, “Nadhani Urusi imekubali pointi hizi mbili. “Nina matumaini makubwa kwamba Ukraine itazikubali,” mjumbe wa Marekani Steve Witkoff pia ametangaza kwenye kituo cha Fox News.
Viongozi hao wawili wamekubaliana kufikiwa kwa makubaliano ya usitishaji mapigano nchini Ukraine, pekee kwa miundombinu ya nishati, ambayo Steve Witkoff amefafanua “inahusu nishati na miundombinu kwa ujumla.”
Wawakilishi hao pia wamebaini kwamba ujumbe wa Marekani nchini Saudi Arabia utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio na Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Mike Waltz.