
Mazungumzo kati ya Ukraine na Marekani kuhusu uwezekano wa kusitisha vita na Urusi yatafanyika leo Jumapili jioni, Machi 23, mjini Riyadh, nchini Saudi Arabia, chanzo ndani ya ujumbe wa Ukraine kimetangaza kwa shirika la habari la AFP.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Mkutano na Marekani umepangwa kufanyika jioni hii,” chanzo hiki cha Ukraine kimeviambia vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na shirika la habari la AFP.
Msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov amesema “mada kuu ya majadiliano” ya Moscow siku ya Jumatatu itakuwa kurejeshwa kwa makubaliano ya nafaka katika Bahari Nyeusi, ambayo yalianza kutekelezwa kati ya mwaka 2022 na 2023. Mazungumzo kati ya Ukraine na Wamarekani yatafanyika Jumapili jioni huko Riyadh.
Mjumbe maalum wa Donald Trump, Steve Witkoff, anasema anatarajia ‘maendeleo ya kweli’ katika mazungumzo ya Saudi Arabia.
“Nadhani mtaona maendeleo ya kweli nchini Saudi Arabia siku ya Jumatatu, hasa kuhusu Bahari Nyeusi,” amesema mjumbe maalum wa Donald Trump, Steve Witkoff, katika mahojiano na kituo cha Fox News, akimaanisha “kusitishwa kwa mapigano baharini kati ya nchi hizo mbili, na kutokana na hilo, kwa kawaida tutaelekea kwenye usitishaji vita kamili.”
“Nadhani anataka amani,” mjumbe wa rais wa Marekani pia amesema kuhusu Vladimir Putin.
Ikiwa Vladimir Putin “amekuwa vitani kwa miaka kadhaa, ni kwa sababu ya maeneo haya matano” ya Ukraine ambayo Urusi imechukua rasmi, Steve Witkoff amebainsha, akisema kwamba “maoni ndani ya Urusi ni kwamba haya ni maeneo ya Urusi, na kwamba kumekuwa na kura za maoni katika maeneo haya, ambayo yanahalalisha vitendo hivi.” “Siegemei upande wowote kwa kusema hivi,” mjumbe huyo ameongeza, “ninatambua matatizo ni nini.”
Siku ya Jumamosi, Bw. Witkoff alimsifu Bw. Putin katika podikasti: “Simchukulii [yeye] mtu mbaya,” alisema kuhusu rais wa Urusi, ambaye aliamuru jeshi lake kushambulia Ukraine mnamo mwaka 2022.
Urusi inasema inatarajia “mazungumzo magumu” na inaamini kuwa “suala kuu” litakuwa “kurejeshwa” kwa makubaliano ya nafaka ya Bahari Nyeusi.
“Hili ni somo gumu sana na kuna kazi kubwa ya kufanywa. “Sisi ni mwanzo tu,” msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov aliambia televisheni ya Urusi kuhusu mazungumzo yenye lengo la kumaliza mzozo nchini Ukraine, kabla ya mazungumzo nchini Saudi Arabia.
Urusi ilijiondoa baada ya mwaka mmoja, ikilalamika kwamba nchi za Magharibi haziheshimu ahadi zake za kupunguza vikwazo kwa usafirishaji wa bidhaa za kilimo na mbolea za Urusi. “Wapatanishi wetu watakuwa tayari kujadili tofauti inayozunguka suala hili,” Peskov ameongeza.