
Kyiv imesema siku ya Jumanne Mei 13 kuwa kutokuwepo kwa Vladimir Putin kwenye mazungumzo kai ya Ukraine na Urusi yaliyopangwa kufanyika Mei 15 mjini Istanbul – ambako Volodymyr Zelensky anatarajiwa kwenda – itakuwa “ishara ya mwisho” kwamba Moscow haitaki kusitisha vita.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
“Ninadhani kwamba ikiwa Vladimir Putin atakataa kwenda Uturuki, itakuwa ishara ya mwisho kwamba Urusi haitaki kumaliza vita hivi, na kwamba haiko tayari kufanya mazungumzo,” Andriy Yermak, mshirika wa karibu wa Bw. Zelensky, katika taarifa kutoka kwa rais wa Ukraine siku ya Jumanne, Mei 13. “Ikiwa Urusi itakataa kufanya mazungumzo, Marekani inapaswa kujibu dhidi ya Urusi: vikwazo vipya dhidi ya Urusi na kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine,” amesema pia..
Haieleweki
Kwa siku mbili, Kremlin imehifadhi muundo wa wajumbe wa Urusi – na uwezekano wa uwepo wa rais wa Urusi – katika mazungumzo haya, ambayo yangeunda majadiliano ya moja kwa moja kati ya Kyiv na Moscow tangu msimu wa 2022, mwanzoni mwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Washirika wa kyiv wa Ulaya walikuwa wamemhimiza Vladimir Putin kukubali usitishaji vita wa siku 30 kuanzia Mei 12. Rais wa Urusi, huku akipuuza wito huu, kisha alitangaza kuwa yuko tayari Jumamosi kwa majadiliano “ya moja kwa moja” kati ya Warusi na Waukreni mnamo Mei 15 huko Istanbul. Volodymyr Zelensky alijibu kwa kujitolea kukutana na Bw. Putin “ana kwa ana” katika jiji hilo hilo.
Lakini Kremlin, kwa siku ya pili mfululizo, ilikataa kutoa maoni juu ya mwaliko wa rais wa Ukraine. “Upande wa Urusi inaendelea kujiandaa kwa mazungumzo yaliyopangwa kufanyika siku ya Alhamisi. Hilo ndilo tunaloweza kusema. “Hatuna mpango wa kutoa maoni zaidi kwa wakati huu,” msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema. Alipoulizwa kuhusu muundo wa timu ya mazungumzo ya Urusi, Bw. Peskov pia amekataa kuzungumza: “Mara tu rais atakapoona ni muhimu, tutatangaza.”
“Sababu kuu za mzozo”
Siku ya Jumamosi, Vladimir Putin “hakuondoa” wazo la kusitisha mapigano kujadiliwa wakati wa mazungumzo ya Istanbul, lakini alisisitiza kwamba, kwa maoni yake, wanapaswa kushughulikia kwanza “sababu kuu za mzozo.” Haya yanaashiria malalamiko ya madai ya Moscow dhidi ya Kyiv na nchi za Magharibi, ambayo Urusi imetaja kuhalalisha uvamizi wake. Haya ni pamoja na lengo la Kremlin la Ukraine kutokuwa na jeshi, kuwalinda wazungumzaji wa Kirusi, na kupinga uanachama wa Kyiv katika NATO, madai ambayo Moscow inatoa kama tishio linalowezekana kwa usalama wake.
Ukraine na washirika wake wa Ulaya wanakataa madai haya, wakisema jeshi la Urusi, ambalo bado linachukua 20% ya ardhi ya Ukraine, linaendesha mzozo wa mtindo wa ubeberu katika jamhuri ya zamani ya Soviet.
Kwa upande wake, Friedrich Merz amebainisha tena Mei 13 kwamba Urusi italengwa na duru mpya ya vikwazo, ikiwa kutakosekana kwa “maendeleo ya kweli wiki hii” katika kutafuta usitishaji vita nchini Ukraine, ameonya kansela mpya wa Ujerumani. Iwapo Moscow “haitaidhinisha” pendekezo la washirika wa Kyiv la kusitisha mapigano kwa siku thelathini, vikwazo vya ziada vilivyotayarishwa na Umoja wa Ulaya “vitaidhinishwa na vitahusu hasa sekta za nishati na soko la fedha,” amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin.