
Serikali ya Uingereza inaonya kwamba mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaweza kuzidi kuwa mzozo mkubwa wa kikanda.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Serikali ya Uingereza imeonya siku ya Jumapili kwamba kuongezeka kwa mashambulizi ya wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuna hatari ya kuzusha “mzozo mkubwa zaidi wa kikanda”.
Wapiganaji wa M23 walilitimua jeshi la Kongo na kuuteka mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Goma mwezi uliopita.
Kisha siku ya Ijumaa, kundi hilo la waasi na wanajeshi wa Rwanda waliandamana kwa kiasi kikubwa bila upinzani kuelekea mkoa wa Kivu Kusini na kuuteka mji wa Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, vyanzo vya usalama na kibinadamu vimesema.
Soma piaMashariki mwa DRC: Nchi za Ulaya zalaani Rwanda kuunga mkono M23
“Kuingia kwa M23 na Vikosi vya Ulinzi vya Rwanda katika mji wa Bukavu ni ukiukaji wa uhuru na uadilifu wa eneo la DRC, na uvunjaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa,” msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza amesema katika taarifa.
“Hili ni ongezeko kubwa ambalo linaongeza hatari ya mzozo mkubwa wa kikanda, ambao gharama yake ya kibinadamu itakuwa mbaya.
“Uingereza inataka kusitishwa mara moja kwa uhasama, kuondolewa kwa jeshi la Rwanda (RDF) katika ardhi ya DRC na kurejea kwa mazungumzo kupitia michakato ya amani inayoongozwa na Afrika. Hakuwezi kuwa na suluhisho la kijeshi. “