
Waziri wa Burundi na chanzo cha misaada ya kibinadamu kimethibitisha siku ya Jumapili kuwasili kwa maelfu ya wakimbizi wa Kongo waliokimbia mapigano kati ya jeshi la DRC, FARDC na waasi wa M23.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Maelfu ya watu wametoroa maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kukimbilia Burundi tangu wapiganaji wa M23, wakishirikiana na wanajeshi wa Rwanda, kuudhibiti mji wa Bukavu, waziri wa Burundi na chanzo cha misaada ya kibinadamu wamesema siku ya Jumapili, Februari 16, 2025. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi Martin Niteretse ameripoti kuwasili kwa “maelfu ya wakimbizi wa Kongo”, lakini akasema idadi yao bado inatathminiwa. “Waliingiwa na hofu waliposikia kuwa jiji la Bukavu limechukuliwa na M23,” Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi Martin Niteretse ameliambia shirika la habari la AFP.
“Tangu siku ya Ijumaa jioni, tumekuwa tukikabiliwa na ujio mkubwa wa wakimbizi wa Kongo,” kimesema chanzo ndani ya shirika lisilo la kiserikali kiliyoko upande wa mpaka wa Burundi. “Kuna watu zaidi ya 10,000 na zaidi wameendelea kuwasili leo,” kimeongea chanzo hiki. Wakimbizi hao walikimbia eneo la Kamanyola huko Kivu Kusini kupitia Mto Ruzisi na kukimbilia katika mkoa wa Burundi wa Cibitoke (kaskazini magharibi), chanzo hicho kimesema.
Baada ya kuteka Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, katika mashambulizi makubwa mwishoni mwa mwezi Januari, waasi wa M23 waliingia katika viunga vyamji wa Bukavu, mji mkuu wa Kivu Kusini, siku ya Ijumaa jioni, ambapo wlichukua udhibiti wa mji huo siku ya Jumapili. Burundi, ambayo jeshi lake linashiriki pamoja na wanajeshi wa DRC katika mzozo huu, ilifunga kwa muda mpaka wake na mashariki mwa DRC siku ya Alhamisi mchana. Vyanzo kadhaa vya Burundi vilitaja wimbi kubwa la Wakongo waliingia katika eneo la Gatumba, ukanda muhimu wa kiuchumi kwa pande zote mbili.