Visiwa vinavyozozaniwa: ICJ yatoa uamuzi kwa Equatorial Guinea dhidi ya Gabon

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imelitoa uamuzi unaoiunga mkono Equatorial Guinea Mei 19, 2025, katika mzozo wa miongo kadhaa kati yake na Gabon kuhusu visiwa vitatu vidogo vilivyoko kwenye maji yanayoweza kuwa na utajiri wa mafuta. Mataifa hayo mawili jirani ya Afrika ya Kati yamekuwa yakipigania Mbanié, kisiwa chenye takriban heka thelathini, na visiwa viwili vidogo, Cocotiers na Conga, tangu mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ni kisiwa chenye takriban heka 30 na visiwa viwili ambavyo, kwa miaka mingi, vimechochea mzozo kati ya mataifa hayo mawili yenye utajiri wa mafuta. Nchi zote mbili zilidai mamlaka juu ya vipande hivi vya ardhi na, haswa, juu ya maji ya eneo linalozizunguka. Maji haya yana uwezekano wa kuwa na mafuta mengi, gesi na samaki… hilo ndilo lilikuwa suala kuu katika suala hili, anakumbusha mwanahabari wetu huko  Hague, Stéphanie Maupas.

Katika kudai mamlaka, kila moja ya mataifa hayo mawili yalidai kuwa na hati ya umiliki. Gabon ilitegemea hasa mkataba ambao Malabo iliuelezea kama “karatasi” wakati wa kusikilizwa kwa kesi huko  Hague mnamo mwezi Oktoba 2024. Majaji waliamua kwamba mkataba huu haukuwa na thamani ya kisheria. Ni vyeti tu vilivyotolewa wakati wa uhuru na Ufaransa kwa Gabon mwaka 1960 na Uhispania kwa Equatorial Guinea mwaka 1968 ndivyo halali, kama ilivyoelezwa na Naibu Mkuu wa Mahakama, Jaji Julia Sebutinde:

“Kwa kuzingatia yaliyotangulia, Mahakama ilihitimisha kwamba tarehe 12 Oktoba 1968, tarehe ya uhuru wa Equatorial Guinea, Uhispania, kama mamlaka ya kikoloni, ilishikilia hati miliki ya Mbanié/Mbañe, Cocotiers/Cocoteros na Conga kwa sababu ya onyesho la kukusudia la mamlaka ambalo lilikuwa endelevu na lisilopingwa kati ya hatimiliki. Kwa hiyo, miongoni mwa vyeti vya kisheria vilivyoombwa na wahusika, cheti ambacho kinatawala katika mahusiano kati yao kuhusiana na mamlaka juu ya visiwa hivi ni cheti ambacho kilishikiliwa na Uhispania tarehe 12 Oktoba 1968, ambacho kiliwasilishwa kwa Equatorial Guinea kwa njia ya mirathi baada ya kupata uhuru wake.

Zaidi ya mafuta, pia kulikuwa na mazungumzo ya upatikanaji wa bahari, ambayo sasa itakuwa ndogo zaidi kwa Gabon. Ingawa waliweka mipaka, kama ilivyoombwa na makubaliano ya pande zote mbili, majaji hawakusema ni nani mwenye mamlaka juu ya visiwa hivi vidogo, lakini nchi zote mbili ziliahidi kutekeleza uamuzi wa Mahakama. Nchi hizo mbili zitalazimika kuendelea na mazungumzo yao kwa msingi uliowekwa wazi wa kisheria.

Katika majibu yake ya kwanza rasmi, serikali ya Gabon imesema ina heshimu uamuzi wa mahakama: “Serikali inabainisha kuwa mbali na kusuluhisha kwa uhakika mzozo kati ya nchi hizo mbili, uamuzi huu unaleta utata zaidi na kuzitaka pande zote mbili kuanza tena mazungumzo,” amesema Laurence Ndong, msemaji wa serikali. Serikali inathibitisha uhusiano wa kina wa Gabon na kanuni ya ujirani mwema, ushirikiano wa kikanda na udugu kati ya watu. “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *