Virusi vya Mpox bado ni tishio la afya kimataifa : WHO

Shirika la afya duniani WHO, limesema virusi vya Mpox bado ni tishio la afya la kimataifa, zaidi ya watu alfu 37 wakiwa wameathirika na virusi hivyo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mkurugezi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ametangaza kuongeza muda wa hali ya dharura wa kubaliana na ugonjwa huo, baada ya mkutano na watalaamu wa kimataifa, ambao wamesema bado kuna ongezeko la maambukizo eneo la Afrika Magharibi na nje ya Afrika.

WHO imesema tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza mwaka uliopita nchini DRC, ugonjwa huo umesambaa kwa mataifa zaidi ya 25, zaidi ya vifo 125 vikiripotiwa, DRC ikiongoza kwa maambukizo na vifo, ikifuatwa kwa karibu na Uganda, Burundi na kisha Sierra Leone.

Shirika hilo la afya duniani sasa linasema linafuatilia mwenendo wa maambukizo, hasa eneo la Afrika ya Magharibi na nchi ya bara, wakati huu baadhi ya mataifa yakiripotiwa kushindwa kufuatilia mwenendo wa maambukizo kutokana na ukosefu wa ufadhili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *